Sunday, September 16, 2012

Mh Tundu Lissu Afiwa na Baba yake

Ninasikitika kuwatangazia kuwa muda mfupi uliopita baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) amefariki katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi, Amina.

Chadema Blog inapenda kuchukua nafasi hii kukupa pole Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na Baba Mzazi. Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki cha Majonzi na Mwenyezi Mungu amlaze mzee wetu Mahali pema Peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment