Ni saa chache zimebaki kabla ya wananchi wa manispaa ya Iringa mjini na viunga yake kukutana na makamanda, wabunge na viongozi wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa mwembetogwa baada ya maandamano ya takribani km 2.
Katika mkutano huo viongozi wataongelea na kujadili maswala mbalimbali yanayo husu mustakabali wa maisha ya wananchi. Aidha pamoja na mambo mengine ziara hiyo ina lengo la kuimarisha na kupanga imara safu za viongozi kuanzia ngazi ya matawi,vitongoji ,mitaa, vijiji, kata, wilaya, majimbo, mikoa, kanda hadi Taifa ikiwa ni maandalizi ya mipango kabambe ya kuchukua dola 2015.
Ni muhimu kufahamu kuwa Iringa mjini ni mojawapo kati ya majimbo Tanzania bara yalichukuliwa kwa kile kinachaitwa "Nguvu ya Umma" dhidi ya nguvu ya dola, makatazo au maelekezo na amri walizokuwa wanapewa Wakurugenzi kutokutangaza matokeo iwapo wapinzani wangeibuka kidedea kama majimbo ya Nyamagana, Arusha mjini, Ubungo, kawe n.k.
Ni muhimu pia kufahamu kuwa Dr. Slaa zaidi ya mara 2 alizuiwa kufanya mikutano katika uwanja wa mwembetogwa kwa kufyatuliwa mabomu na risasi za moto. Ni imani yangu kuwa "Justice shall always prevail" karibuni Iringa wakombozi wetu.
No comments:
Post a Comment