Sunday, August 19, 2012

Lema afungua matawi ya CHADEMA Daraja Mbili Arusha na kuvua magamba


Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Katika ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.
Mbali na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
Akiondoka eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake  ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi ya watu wakinyoosha vidole  kama ishara ya ushindi.




No comments:

Post a Comment