Monday, August 27, 2012

ASEMAVYO MWANACHADEMA KUHUSU MAUAJI YA RAIA MOROGORO

Tunalaani vikali mauaji yaliyofanywa leo na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro katika harakati za kuzuia Maandamano ya amani ya CHADEMA. Ikumbukwe kuwa tulitaka kuzindua Operesheni Sangara tarehe 08/08/2012 Morogoro Mjini, RPC akakataa kwa sababu ya sherehe za nane. Baada ya majidiliano ya viungozi wetu Wakuu na IGP tulikubaliana kwenda kuzindua Operesheni yetu Jimbo la Kilombero-Ifakara kwa makubali
ano kuwa tutafungia Operesheni yetu Morogoro Mjini kwa maandamano.

Tulipotaka kufunga jana tarehe 26/08/2012 busara ikatushauri tupishe zoezi la sensa na tufunge tarehe 27/08/2012 na tukakubaliana na RPC hivyo tarehe 25/08/2012. Jana jioni ndio RPC anakataa kusiwe na maandamano na badala yake viongozi ndio wawe kwenye msafara wa magari kwani eti shughuli za Morogoro zitasimama. Alipokumbushwa makubaliano akawa na kiburi cha Madaraka.

Leo asubuhi wakati watu wanakusanyika ili wajue namna ya kufanya ndipo Polisi wakaanza kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na Risasi za Moto hadi kuuwa raia. MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU ALLY ZONA PEPONI. DAMU YAKO HAIJAMWAGIKA BURE KAMANDA ITAKUWA SABABU YA UKOMBOZI WA TAIFA HILI


PANTALEO ANSELEM 

ChANZO Facebook

No comments:

Post a Comment