WIMBI la mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaloendelea kwa kuendesha mikutano mbalimbali nchini, safari hii limemshukia Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) na kumfananisha na ‘tikitimaji’.
Katika mkutano huo, ambao ulihutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho ambaye pia alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UVCCM), James Ole Millya, walimlaumu ole Sendeka kuwa ameshindwa kupeleka maendeleo katika Jimbo lake, tofauti na maneno anayotoa.
Katika mkutano huo, Chadema walitumia usafiri wa helikopta (chopa), ambayo ilionekana kuwa kivutio kwa wakazi wa Simanjirio na vitongoji vyake.
Viongozi wengine waliohutubia kwenye mikutano hiyo ni pamoja na aliyekuwa diwani wa Sombetini kwa tiketi ya CCM, ambaye hivi karibuni alihamia Chadema, Alphonce Mawazo na aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa CCM na UVCCM, Ally Bananga.
Katika mkutano huo, wanachama 1,200 kutoka CCM, walijiunga na Chadema.
Wanachama hao wa CCM, walirudisha kadi pamoja na sare za chama hicho, zikiwemo fulana, bendera na vitambaa vya kichwa katika mikutano iliyofanyika kwenye maeneo ya Narekauo, Lolbosiret, Naberera, Ndovu, Orkesument na Marerani
Mtanzania
No comments:
Post a Comment