Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amesema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kurejesha heshima ya Bunge kwa ukamilifu, mbali na uamuzi uliofikiwa na spika wa kukubali kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na madini.
Mnyika ameyasema hayo kupitia kwenye waraka wake alioutoa juzi kwa minajili ya kutoa maoni yake kuhusiana na hatua ya Bunge ya kuivunja kamati hiyo ya kudumu kutokana na kukumbwa na tuhuma nyingi za rushwa.
“Kwa maoni yangu uamuzi huo ni sahihi lakini umechelewa na pekee hauwezi kurejesha heshima ya bunge kwa ukamilifu wala hautaweza kushughulikia uzembe na udhaifu ulioko kwenye Bunge na kwenye serikali ikiwa hautaambatana na hatua nyingine za ziada na za haraka,” alisema.
Mnyika alisema kwamba mbali na wabunge wanaodaiwa kupokea rushwa, kuwa na maslahi kwenye wizara, taasisi au mashirika wanayoyasimamia kwenye kamati mbalimbali, heshima ya bunge imeathiriwa pia na maamuzi yasiyo na tija kama yale ya kuchaguliwa kwa Andrew Chenge kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, wakati ni mtuhumiwa wa ufisadi wa rada.
Alisema ili kurejesha heshima ya Bunge hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuvunja kamati zote zenye wajumbe waliotuhumiwa kwa rushwa na kufanya mabadiliko makubwa ya wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu za Bunge ili kupunguza maslahi ya kifedha na tuhuma za rushwa miongoni mwa wajumbe wa kamati.
Aidha, aliitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumaliza kazi yake kwa dharura ili majina ya wahusika waliotuhumiwa kwa rushwa yaweze kutajwa ndani ya Bunge na Bunge lipate nafasi ya kujadili na kupitisha maazimio ya hatua za ziada za kuchukuliwa na vyombo huru vya kiuchunguzi na hatimaye watakaothibitika kuvunja sheria wafikishwe mahakamani.
Mnyika alisema pamoja na hatua hizo, kamati za vyama wanakotoka watuhumiwa nazo zichukue hatua kwa wabunge wake watakaotajwa ili kudumisha misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa maslahi ya umma.
Hata hivyo Mnyika alisema Bunge linaweza kujinasua kwenye uzembe ikiwa litatimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali kwa mujibu wa ibara ya 63 kwa kuondoa udhaifu wa serikali kwenye sekta ya nishati na sekta nyingine muhimu za taifa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment