WAKAZI wa Kibwegere, Kata ya Kibamba Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wameaswa kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ili kiwaletee maendeleo ya kweli.
Nasaha hizo zimetolewa jijini jana, katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya kitongoji cha Manzese,na Diwani wa Kata ya Saranga Efraim Kinyafu (Chadema), ambaye ameteuliwa na chama chake kuwa mlezi wa kata hiyo,
Katika mkutano huo, Kinyafu alisema iwapo wakazi hao watakubali mabadiliko ya uongozi kwa kukiunga mkono Chadema kwa asilimia mia moja uhakika wa kuyapatia ufumbuzi matatizo yao utapatikana.
Alibainisha kuwa matatizo yote yanayowakabili wakazi hao yakiwemo ya elimu duni, huduma mbovu ya upatikanaji wa maji na miundombinu mibovu ya barabara havikuja vyenyewe bali vimesababishwa na utawala mbaya wa Chama cha Mapinduzi (CCM), usiojali maslahi ya wananchi.
“Jipangeni kukiunga mkono Chadema haswa kwa kuwachagua viongozi wake kuanzia ngazi za shini hadi Ikulu, ambapo tuanziye na serikali za mitaa mwaka 2014 kisha udiwani, ubunge na urais mwaka 2015, hapo Kichaguweni kiwaondolee kero zenu zote”alisema Kinyafu.
Alisema hadi sasa nchi hii inakabiliwa na tatizo la uongozi bora kutokana na viongozi wengi walioko madarakani kufikiria matumbo yao kwanza.
Naye katibu wa chama hicho Vitalis Muro, wakati akikabidhi kadi kwa wanachama wapya 50 waliyokihama Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema inasikitisha kusikia kuwa kuna baadhi ya wakazi wa eneo hilo hawamjui diwani wa Kata kutokana na kushindwa kwake kuitisha mkutano tangu achaguliwe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho.
Vile vile aliwataka wakazi baadhi ya wakazi wengine kujitokeza katika kujiunga na chama hicho ambacho kimenuia kuwakomboa kutoka kwenye utawala wa kifisadi.
Chanzo Full Shangwe Blog
No comments:
Post a Comment