MUNGU AUWEKE MAHALI PEMA PEPONI MWILI WA MZEE WETU MUSOBI MAGENI, AMEN.
Tuesday, June 5, 2012
MH LETICIA NYERERE AFIWA NA BABA YAKE MZAZI
Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC linachukua nafasi hii kutoa pole kwa Mh Leticia Nyerere kwa kufiwa na Baba yake Mzazi Mzee MUSOBI MAGENI. Mzee Mageni ambaye amewahi kushika Nyadhifa mbalimbali za Serikali kama Uwaziri, Ubunge na Ukuu wa Wilaya kadhaa amezikwa Kijijini kwao Kwimba, Mwanza. Mzee Mageni amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, akiwa mmoja wa Waasisi wa Chama hicho. Chadema Washington DC tumepata taarifa hizi kwa mshtuko mkubwa kwani kabla ya Msiba wa Baba yake Mzazi tulikuwa na Mh Leticia Nyerere katika uzinduzi wa Tawi la Chadema la Washington DC ambapo yeye Mh Leticia Nyerere ndiye aliyeratibu Sherehe za Uzinduzi wa Tawi na mara aliporudi Tanzania ndipo alipokutana na Msiba wa Baba yake Mzazi Mzee Musobi Mageni. Tunachukua nafasi hii kukupa Pole Sana Tupo nawe katika kipindi hiki cha Majonzi. Pia tunachukua nafasi hii kuwapa pole Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF kwa kuondokewa na muasisi wa Chama Chao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment