Friday, June 29, 2012

Kutekwa, kuteswa, kupigwa na kujeruiwa Dkt. Ulimboka kuna harufu ya faulo!

Nchi ya Tanzania imeshuhudia tukio la kinyama na la ki-mafia kuliko yote yaliyopata tokea hapa nchini. 

Kutokana na kuendelea kwa mgomo wa Madaktari nchini, nani hatokuwa na wasiwasi kuwa kutekwa, kuteswa na hatimaye kupigwa kinyama kwa Dkt. Ulimboka Steven ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madaktari nchini, umoja ambao ndio unaongoiza mgomo wa Madaktari?

Tumepata kusikia minong'ono kuwa viongozi wengi wa Chama na Serikali waliokwenda kinyume na matakwa ya wakubwa wao ama walikufwa katika mazingira ya kutatanisha au walienda gerezani kunyea debe. Mifano hai ipo na mwingine hivi sasa ni kiongozi mkubwa tu hapa katika Jamhuri ya Muungano. 

Suala la kunyofolewa kucha Dkt. Ulimboka inaonesha wazi waliomtesa ni watu wenye mafunzo ya kutesa watu na wanaojua wanachokifanya. Cha kujiuliza ni je, wewe msomaji wangu, watu aina hiyo wanapatikana katika viwanda vya watu binafsi au katika Idara nyeti za Usalama ambazo huwa chini ya Serikali? 

Hata sijui tunaendea wapi na vitendo hivi vya ki Mafia. 

Tukio hili linarudisha nyuma mpaka mwaka Jan/2010 ambako kaka yangu Swetu Fundikira alitekwa nyara na Askari Jeshi watatu kutoka maeneo ya Kinondoni na saa moja baadaye wakakutwa naye maeneo ya Upanga Jamatini akiwa uchi wa mnyama na hana fahamu kwa kipigo, na baadae alifariki hapo Muhimbili Hospitali kwa majeraha ya kichwa.

Chanzo - Wavuti

No comments:

Post a Comment