Saturday, June 2, 2012

Dk Slaa amshukia mama Anna Mkapa

Aidha, Dk Slaa alisema serikali kwa kujua iliamua kwa makusudi kumuuziauza kiwanda pekee  cha korosho kilichopo mkoani Mtwara  kwa sh. milioni 50 na kuwaacha wakazi wa mtwara wakihangaika na korosho zao pasipo kujua ni wapi watazipeleka.
Alisema kama kiwanda hicho  kingeachwa wakazi wa Mtwara wasingekuwa na taabu ya kujua ni wapi pa kupeleka korosho zao.
“Taarifa nilizonazo kiwanda hicho alichouziwa mama Mkapa kimeondolewa mitambo yote na sasa kimebaki tupu na hakuna kinachoendelea juu ya hilo huku ninyi mkibaki na umasikini wenu”alisema Dk Slaa
ATAKA MAAFISA USALAMA  WA TAIFA WARIPOTI KWAKE
Akizungumzia hali ya usalama Dk Slaa alisema kuanzia sasa ni lazima maafisa hao wakaripti kwake kila atakapokuwa akifanya mikutano kwa kuwa huo ndiyo wajibu wao.
Alisema kazi ya polisi ni kufanya kazi ya kulinda wananchi na usalama wa taifa wanawajibu wa kuangalia usalama kwa ujumla na katika taratibu hizo ni lazima wawasiliane naye kabla ya mikutano hiyo kuanza.
Aliongeza maagizo hayo ni kwa mujibu wa sheria ya  vyama vya siasa ya mwaka 2005 inayoelekeza wajibu wa maafisa wa usalama wa Taifa.
MNYIKA ASHANGAA MAJIMBO YA WENZAKE
Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa ubungo John Mnyika alisema kilichomvuta kufika katika majimbo ya wenzake ni kuona wamefanya maendeleo kiasi gani hata kuamua kuwa mabubu wanapokuwa bungeni.
Alisema ukimya wa wabunge hao ulimfanya kila siku awe anpiga kelele kwa ajili ya mahitaji muhimu ya wananchi kwa kile alichoamini kuwa wenzake wako mbali kimaendeleo.
“Nilijua kuna maendeleo zaidi ya majimbo yetu ya Dar lakini katika haya niliyoyaona nimekosa hata hamu ya kuwa pamoja na hao mliowachagua kuwa wawakilishi wenu”alisema Mnyika
HECHE AZUNGUMZIA UDINI
Mwenyekiti wa Taifa wa Bavicha John Heche akihutubia katika kata ya Namikupa Tandahimba alisema propaganda za udini zinazoelekezwa kwa chama chake ni mawazo ya watu waliofilisika kisiasa.
Alibainisha kuwa hata mtu akiwa ni kiongozi kutoka katika dini inayowahusu na hafuati maagizo ya dini kuwakomboa wananchi basi dini yake haitakuwa na maana kwa jamii inayomzunguka.
WANANCH WAMKATAA MBUNGE TANDAHIMBA
Katika hali isiyo ya kawaida maeneo mbali mbali kulipofanyika mikutano ya hadhara wananchi walipiga kura ya kumkataa mbunge wao Juma Njuwayo huku wengine wakisema hawamjui wala hawataki kumuona.
Wakazi wa Namipuka walisema mara ya mwisho kuonekana kwa mbunge huyo ni pale alipofika kuwaomba kura na baada ya hapo hajawahi kuonekana tena huku wakiomba uchaguzi mwingine ufanyike katika jimbo lao kwa ajili ya kupata mtu wa kuwasemea.
Katika uwanja wa Tandahimba kila mara lilipotajwa jina la mbunge huyo wananchi walisema hatumtaki ameiba kura hatumtaki hatuna mbunge huyo ni mbunge wa ccm na siyo wetu sisi

No comments:

Post a Comment