Friday, May 25, 2012

RAI:TUWATUNZE NA TUWAIFADHI KABILA LA HADZABE

Hadzabe ni kabila maarufu sana kupita yote Duniani.Kisayansi na pia kwa kutumia DNAmedhibitwa kuwa binadamu wa kwanza ametoka kwenye hili kabila.Watu wote duniani  awe mchina,mzungu,mspenishi wote kwa kutumia technologia ya hali ya juu imedhitishwa asili yao ni Eyasi hapa Tanzania[east africa].Inasikitisha kuwa wadzabe wanapata shida na kunyanyaswa na serikali ya CCM,bila ya kujua umuhimu wa kabila hilo Duniani.Tumewapa dhamana na madaraka watu wenye roho mbaya ,ubinafsi uchoyo na ukatili.Na kufikia kuuza ardhi ya hawa ndugu zetu na asili ya babu zetu wote hapa Duniani.Eti kwa kisingizio cha miradi ya maendeleo,eti wanawajenga shule,barabara na miradi mingine.Wamewapa ardhi kubwa " UAE ROYAL FAMILY"  KWA AJILI YA UWINDAJI BINAFSI[private hunting] eneo la mraba  maili 2500.Na kuwafanya jamaa zetu wadzabe washindwe kuwinda ndani ya eneo lao.Na wakifanya hivyo wanakamatwa na kupelekwa jela.Na wamepelekwa wengi jela.Sasa kweli watanzania ebu tufikirie kwa makini,kuwanyang'anya ardhi hawa ndugu zetu eti kwa ajili ujenzi wa shule na ,barabara na hospitali???????.Hivi sehemu nyingine watu wanafanyiwa hivyo hivyo?????????.Kama serikali inaweza kunua magali ya bei mbaya inashindwa nini kujenga shule na hospitali???????.Mimi nasema hapana,wahadzabe leo wakisema wasikika kilio chao,kuwa wanataka shule ,hopitali,na miradi mingine nakuambia kutapatikana michango mingi sana Dunia nzima kwa ajili ya maendeleo yao na huku wakitunza mila zao, na tena mafisadi nao watachanganyikiwa.Kwani kila mtu duniani inamgusa kuwa babu yake katokea kwenye kabila hilo.Sasa serikali Hisio makini ya CCM inazidi kuwamaliza ,na tutambue hawa ndugu zetu wamebakia sio zaidi ya 25,000 .Tumeona UAE ni muhimu zaidi kuliko hawa ndugu zetu.Naomba angalia video hapo juu.NAOMBA WATANZANIA TUFUATILIE KWA UNDANI KAMA KUNA WADZABE WAPO JELA ,TUSIMAME IMARA NA KUWATOA.NAOMBA WATANZANIA TUSIWE NA HURUMA NA CCM ,TUWANG'OE 2015 KWA KURA ZETU.NAOMBA KILA KIJANA ATUNZE HATI YAKE YA KUPIGA KURA,NA KAMA HANA AKACHUKUE SASA HIVI,KWANI HATUNA MUDA TENA.PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO,PAWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA,HATULALI MPAKA KIELEWEKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WENYE BUSARA YA KUTAZAMA MBELE.

Ludigo Mhagama[environmentalist]

No comments:

Post a Comment