CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kimependekeza kuwapo kwa serikali tatu katika Katiba mpya.
Mwenyekiti wa muda wa chama hicho, Wales Mayunga, alieleza hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo yao kwenye Katiba mpya.
“Katika mapendekezo yetu tumeeleza kuwa serikali ziwe tatu ila ‘Serikali ya Tanzania Bara’ lifutwe na kuitwa Serikali ya Tanganyika, kwani hakuna na hakutakuwepo serikali ya Tanzania Bara.
Alisema katika serikali hiyo wamependekeza kuwapo kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Tanganyika na Waziri Mkuu wa Zanzibar.
Katika mkutano huo, chama hicho kilitambulisha baadhi ya wanachama wake wapya akiwamo Alhaji Hashim Sipunda Rungwe aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Hassan Mbwana, aliyekuwa Kamishna wa Mkoa wa Tanga NCCR Mageuzi.
Akielezea sababu za kukihama chama hicho Alhaji Rungwe alisema ni masharti makali aliyopewa na viongozi wa NCCR kumtaka asikishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment