Dr. Wilbroad Slaa, amealikwa kwa
mahojiano na WPFW Radio ya Washington, D.C. U.S.A. siku ya jumatano
tarehe 13 Machi, 2013. Saa saba mchana, saa za Amerika ya mashariki ( 1pm U.S
Eastern time)/ Saa mbili usiku saa za Afrika mashariki (8pm East Africa time).
Kumefanyika jitihada za kuushirikisha ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
kushiriki mahojiano haya bila kuwa na mafanikio. Bado jitihada za kuushirikisha
ubalozi zinafanyika.
Baadhi ya mambo yatakayo jadiliwa ni
hali ya siasa Tanzania, hali ya kijamii, hali ya kiuchumi, amani na usalama wa
Tanzania na mengineo.
Bofya hapa kusikiliza WPFW radio
live WPFW Radio
No comments:
Post a Comment