JAJI WARIOBA KUKUTANA NA WANAHABARI KESHO ALHAMISI, MACHI 7, SAA 4:00 ASUBUHI
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba atakutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam, kesho (Alhamisi, Machi 7, 2013) kuanzia saa 4:00 asubuhi. Katika mkutano huo, Jaji Warioba atazungumzia uundwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Waandishi wa Habari wa
vyombo vyote mnakaribishwa.
No comments:
Post a Comment