Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuwabaini watu waliohusika kumfanyia vitendo vya kikatili Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Hatua ya Jaji Warioba imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Kibanda kufanyiwa vitendo vya kinyama na watu wasiojulikana na kumjeruhi. Kibanda kwa sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Mbali na hilo, Warioba alisema kitendo hicho kinaonyesha wazi kwamba tukio hilo si la ujambazi,bali ni kama njama zilizopangwa na baadhi ya watu waliokuwa na lengo la kumdhuru.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema kitendo alichofanyiwa Kibanda ni cha kinyama na kwamba hakiwezi kuvumilika kwani kinasikitisha na kinahuzunisha kwa kila mtu.
ìKama hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti vitendo kama hivyo, matukio hayo yanaweza kuendelea kwa waandishi wa habari kushambuliwa.îalisema Warioba.
Alisema kwa jinsi kitendo hicho kilivyofanyika kwa Kibanda, kinaonyesha wazi kwamba watu waliomshambulia Kibanda walikuwa sio majambazi bali ni watu waliopanga njama ili kumjeruhi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment