Sunday, December 30, 2012

Kaya zaidi ya 150 wamekihama CCM na kujiunga na CHADEMA

Wanakaya zaidi ya 150 wa kijiji cha Ambureni/Moivarowameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kuchoshwa na ufisadi unaofanywa naSerikali ya chama cha mapinduzi.
Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari waliohudhuriakwenda kusikiliza kero zinazowakabili wanakijiji wa Ambureni.
Wananchi hao walilalamika kuwa wamekuwa wakilazimishwakuchangia michango ya shughuli za maendeleo ya kijiji kama vile ujenzi wa choocha shule, lakini tangia walipoanza kuchangishwa mpaka leo hii serikali yakijiji imeshindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi.
Kila mwanakijiji alichangishwa Shilingi 15,000 kwa kilakaya. Kwa mujibu wa taarifa za mwenyekiti wa serikali ya kijiji, kayazilizochangia kiasi cha fedha ni kaya 600, ambapo kwa mujibu wa wakazi wakijiji hicho cha Ambureni wamedai kuwa kijiji kina kaya zaidi ya 1500, takwimuhii ya kaya 1500 inatokana na Daftari la kupiga kura la mwaka 2010. Hata hivyo,kwa mujibu wa wanakijiji cha Ambureni, baada ya 2010 kuna wageni wengiwalioongezeka, jambo linaloashiria kuwa kwa sasa Ambureni kuna kaya zaidi ya1500.
Hivyo, kutokana na takwimu hizo wanakijiji hao walitegemeakuwa kiasi cha mchango wa zaidi yashilingi 15,000 x 1,500 = 22,500,000/=.
Michango hii ni nje ya mauzo ya viwanja/mashamba ambayoserikali ya kijiji huchukua 10% kwa kila mauzo.
Pia kuna mapato yanayotoka halmashauri kwa ajili ya shughuliza maendeleo ya kijiji.
TANAPA walitoa mil. 12.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji alikiri kuwa kaya 600zilichangia mchango wa 15,000 kwa kila kaya, ikakusanywa shilingi 9,000,000/=.Pia waliamrishwa kuchangia tena kila kaya kuchangia 26,000/= kwa ajili yaujenzi wa choo cha shule. Ambapo wanakijiji waligoma kuchangia, wakitaka kujuamapato na matumizi ya fedha kwa miaka 12 tangu mwenyekiti alipoingiamadarakani. Hapo ndipo vitisho vilipoanza akidai kuwa watakaouliza maswalikuhusu mapato na matumizi wanaweza kukamatwa na kupelekwa polisi, kwa kuwasuala la mapato na matumizi chama kinafahamu.
Wanakijiji walipeleka malalamiko kwa mkuu wa wilaya, baadaya kuona malalamiko yao hayashughulikiwi ngazi za chini.
Mkuu wa wilaya akaliona suala kama jepesi, kwani alimtumaafisa masoko kwenda kwenye mkutano wa wananchi na mwenyekiti wa kijiji, ambapowananchi walimkataa afisa masoko, wakidai hawafanyi biashara, pia kuwawangemkataa mwenyekiti wa kijiji ambaye ndiye mtuhumiwa wa ufisadi wa fedha zawanakijiji nani angemwajibisha kama wakubwa wake wote hawapo. Mkutano huoulivunjika huku mwenyekiti huyo akiwarushia maneno wanakijiji kuwa hakunamwenye uwezo wa kumwondoa kwenye kiti hicho, kwani mambo yote chama chake (ccm)kinafahamu.
Mkuu wa wilaya alimtuma Mkaguzi wa Halmashauri kufanyaukaguzi, ambapo taarifa za mkaguzi zilionyesha kuwa fedha zilizokusanywa nishilingi 1,052,000/=. Taarifa hii inapingana na ripoti ya mwenyekiti wa kijijizilizoonyesha kuwa kaya 600 ndizo zilizochangia shilingi 15,000 kwa kila kaya,kama attachment zinavyoonyesha.
Wananchi wamepinga kuwa kaya zilichochanga michango ya15,000 ni zaidi ya 600 na siyo 600, wananchi wamehoji iweje kwenye shughulizingine kuwe na idadi ya kaya zaidi ya 600, lakini linapokuja kwenye suala lamapato na matumizi kaya ziwe 600?

No comments:

Post a Comment