Wednesday, May 30, 2012

OPERESHENI Okoa Kusini ya CHADEMA yashika kasi

Baada ya jana kufanya mikutano ya hadhara, kufungua matawi na kuweka uongozi wa muda kata zote 15 za Wilaya ya Mtwara Mjini, leo Operesheni Okoa Kusini imeingia vijijini.

Ratiba ya leo Wilaya ya Mtwara Vijijini ni ifuatavyo: Timu ya Mwenyekiti Freeman Mbowe itakuwa Kata za Madimba na Tangazo, Timu ya Makamu Mwenyekiti Said Mohamed Issa itakuwa Kata za Msanga Mkuu na Ziwani, Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa itakuwa Mtimbilimbwi na Nanyamba, Timu ya John Mnyika itakuwa Nanguruwe na Mayanga, Timu ya Tundu Lissu itakuwa Nitekela na Milangominne, Timu ya John Heche itakuwa Bilimba na Mnima, Timu ya Godbless Lema itakuwa Mtinjiko na Mbembaleo, Timu ya Ezekia Wenje itakuwa Kata za Kitere na Libobe.

Kazi ni ile ile mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, kufungua matawi, kusimika uongozi wa muda kuelekea uchaguzi wa ndani kuanzia Juni 1 mwaka huu!

Kujenga oganaizesheni ya chama kuanzia vijijini mpaka mjini, kueneza elimu ya uraia, hasa suala la katiba mpya, kuendelea kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi katika ngazi zote hasa ktk kushughulikia vyanzo vya matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, yanayoikabili nchi kwa sasa, badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo hayo kama inavyofanywa na serikali ya CCM hivi sasa.

No comments:

Post a Comment