Friday, May 31, 2013

KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI!!!


TAARIFA KWA UMMA

KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI!!!

Dar es Salaam, 31 Mei 2013...

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali njama za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amedai kwamba CHADEMA imekamata nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliowakuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Mh. Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu. Kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27 Aprili mwaka jana.

Dr. Slaa alisema kwamba lengo la njama za Kinana na CCM ni kuhakikisha kwamba Mh. Lissu anafutiwa Ubunge ili asiweze kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya kama mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha rasimu ya Katiba Mpya baadaye mwaka huu. Dr. Slaa alisema: “Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge, Mheshimiwa Lissu amekuwa mwiba mkali kwa CCM na Serikali yake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Amefumbua macho ya mamilioni ya Watanzania kuhusu masuala makubwa ya kikatiba na kisheria kwa hoja zake Bungeni. Uelewa wake mpana wa masuala hayo na wa Kanuni za Bunge umekuwa kikwazo kikubwa kwa CCM na Serikali yake pamoja na uongozi wa Bunge kupitisha mambo yao kinyume cha sheria, Kanuni za Bunge na maslahi ya nchi yetu. Uwepo wake ndani ya Bunge na ujasiri wake katika kutetea hoja mbali mbali umemzuia Spika wa Bunge na uongozi mzima wa Bunge kuwaonea Wabunge wa Upinzani na hasa CHADEMA. Mtu huyu amekuwa adui mkubwa wa CCM ndio maana Kinana anataka aondolewe Bungeni ili asiwepo kabisa katika mjadala wa Katiba Mpya Bungeni.”

Kwa mujibu wa Dr. Slaa, mara baada ya Mh. Lissu kuwasilisha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria tarehe 3 mwezi huu ambapo aliishambulia Tume ya Mabadiliko ya Katiba na CCM kwa kuvuruga mchakato wa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa lengo la kuhakikisha Mabaraza hayo yanakuwa ya wanachama wa CCM tu, Kinana alimwita wakili wa kujitegemea Godfrey Wassonga wa kampuni ya mawakili ya Wassonga Associates Advocates ya mjini Dodoma na kumwelekeza afungue rufaa dhidi ya Lissu katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania haraka iwezekanavyo. Siku nne baadaye yaani tarehe 7 Mei, 2013, Wakili Wassonga alifungua rufaa hiyo katika Masjala Ndogo ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mjini Dodoma.


Ijapokuwa rufaa hiyo inaonyesha kufunguliwa na Shabani Itambu Selema na Paschal Marcel Hallu waliokuwa walalamikaji katika kesi iliyotupwa na Mahakama Kuu, Dr. Slaa alidai kwamba watu hao hawahusiki kwa namna yoyote ile na kufunguliwa kwa rufaa hiyo. 

“CCM na mawakili wao wanawatumia tu wanakijiji hawa bila hata kuwapa taarifa au kuwashirikisha kwa namna nyingine yoyote. Huyu Shabani Itambu Selema amekula kiapo mahakamani Dodoma kwamba yeye na mwenzake ambaye bado ni Katibu Kata wa CCM huko kwao, hawakuambiwa chochote juu ya kufunguliwa kwa rufaa hiyo. Hawakutoa maagizo yoyote kwa Wakili Wassonga kufungua rufaa kwa niaba yao dhidi ya Lissu; hawajamruhusu Wakili huyo kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu iliyoridhika kwamba uchaguzi wa Mbunge Lissu ulikuwa halali; hawajamlipa Wakili Wassonga kwa ajili hiyo. Huyu Wakili anafunguaje kesi au rufaa bila kuambiwa au kulipwa na ‘wateja’ wake? Kama huku sio kukosa maadili ya kiuwakili ni kitu gani?”, amehoji Dr. Slaa.

Kuhusu ushiriki wa Kinana katika sakata hilo, Dr. Slaa alisema kwamba mara baada ya rufaa hiyo kufunguliwa, Wakili Wassonga alimwandikia Katibu Mkuu huyo wa CCM barua yenye kumbu kumbu Na. NO/KM/CCM/01/2013 kwa ajili ya “MADAI YA MALIPO YA AWALI YA SHAURI LA RUFAA KESI YA UCHAGUZI JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI SHABANI ITAMBU SELEMA NA MWENZAKE DHIDI YA MH. TUNDU LISSU.” Barua hiyo inamkumbusha Kinana juu ya ‘makubaliano’ kati ya Wassonga Associates Advocates na CCM kuhusu kusimamia kesi ya wanachama hao wa CCM dhidi ya Mh. Lissu ambayo baadae ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.

“Baada ya shauri husika nilipata maelekezo kutoka kwa wanasheria wa CCM kwamba tukate rufaa Mahakama ya Rufaa kazi ambayo tumekamilisha.” Wakili Wassonga anamweleza Kinana “... katika shauri la mwanzo nilikuwa nalipwa na CCM Singida Mkoa na hawakumalizia malipo.” Barua hiyo imeambatana na hati ya madai ya malipo (invoice) kwa ajili ya ‘malipo ya awali’ ya shilingi milioni mbili.


Dr. Slaa alidai kwamba kazi ya Lissu na wabunge wa CHADEMA ndani ya Bunge inawatisha CCM na Serikali yake ndio maana sasa Kinana anataka Lissu aenguliwe kwa kutumia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. “CCM inatapatapa, Bungeni hapakaliki kwa sababu ya hoja za Lissu na Wabunge wengine wa CHADEMA. Kila siku Bunge linaahirishwa ili kukwepa mijadala mikubwa juu ya matukio muhimu yanayoisibu nchi yetu. 

Njama za kuizima CHADEMA kwa kuipunguzia muda wa kuzungumza Bungeni zimeshindikana; mikakati ya kuvuruga hoja za CHADEMA kwa kuingilia hotuba za Kambi Rasmi ya Upinzani na kutaka sehemu za hotuba hizo zifutwe zimegonga mwamba; vitisho vya Spika Makinda na Naibu Spika Ndugai kuwasimamisha wabunge wetu hazijafua dafu. Sasa tuna taarifa kwamba Kinana anataka kuwahonga majaji ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mamilioni ya fedha ili wamfutie Kamanda wetu Lissu ubunge. Naye atashindwa pia.”

Akizungumzia hati ya kiapo ya Shabani Itambu Selema ambaye alihama CCM na kujiunga na CHADEMA baada ya kesi yao kutupiliwa mbali na Mahakama Kuu mwaka jana, Dr. Slaa amesema:

Bonyeza Read More Kuendelea

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. SYLVESTER MHOJA KASULUMBAYI (MB) KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2012/13 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9), ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Mwaka 2013)

A: UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, dira ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ni kuhakikisha kuwa raslimali za mifugo na uvuvi zinaendelezwa na kutunzwa katika mazingira endelevu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.  Aidha dira inalenga kuhamasisha ufugaji wa kisasa na uvuvi endelevu ili kujenga uchumi endelevu kwa jamii nzima ya wafugaji na wavuvi na taifa kwa jumla.
Mheshimiwa Spika, Licha ya ukweli kwamba wafugaji na wavuvi wana mchango mkubwa katika uchumi wetu, Serikali hii ya CCM imeshindwa kuwapatia maeneo maalum kwa ajili ya malisho kwa maendeleo ya mifugo yao. Wafugaji wamekuwa wakihamishwa na au wakifukuzwa kutoka eneo moja la nchi hadi eneo lingine kama vile hawana haki ya kufanya shughuli za kiuchumi kama ufugaji katika nchi yao. Ni aibu kwa  Serikali kushindwa kuwapatia wafugaji mahitaji muhimu ambayo yangepelekea ufugaji wao kuwa wa kisasa, kibiashara na endelevu kama ilivyobainisha katika dira ya Wizara hii.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, haioni sababu ya Serikali kuwapatia wafugaji maeneo ya kufugia  kwa kuwa wafugaji wangeweza  kuingia ubia na mashamba makubwa ya mifugo ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Ranchi za Taifa, lakini kutokana na ubinafsi na ufisadi uliofichwa kwenye kivuli cha cha sera ya ubinafsishaji,  Serikali ya CCM imesimamia zoezi la  viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi wakigawiana ranchi hizo na kuwaacha wafugaji wakifukuzwa ovyo na kupewa jina la wachungaji.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wavuvi hali ni hiyo hiyo,  kwani mapato mengi ya Serikali  yanayokusanywa kutoka katika sekta ya uvuvi yanatokana na wavuvi wadogo ambao mara zote wao ndio waathirika wa mfumo kandamizi wa Serikali.  Zana za uvuvi zinapokamatwa, wao ndio wanapata hasara, lakini wauzaji wa zana hizo za uvuvi  wala hawaulizwi na wala hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yao.
 Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa inayozikabili sekta hizi za ufugaji na uvuvi ni kwamba sekta  zote mbili hazina bima dhidi ya  majanga ambayo yanaweza kutokea.  Katika mazingira kama haya, dhana ya kuwa sekta za kisasa, kibiashara na endelevu inakuwa ngumu sana.
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa mwaka wa fedha 2012/2013 liainisha mapungufu makubwa katika ya kiutendaji na kiuwajibikaji kwa wizara hii na kuitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo:
1.      Kuwajibika kwa uzembe wa kuitelekeza meli ya uvuvi ya Tawariq iliyokamatwa ikifanya uvuvi haramu katika ukanda wa bahari ya hindi hadi meli hiyo kuharibika kabisa na kuanza kuzama bila faida yoyote?
2.      Kuchukua hatua dhidi ya mwekazaji wa Kagera Sugar kwa kushindwa kuendeleza shamba la ukubwa wa hekta 45,000 (sawa na ekari 112,500) kinyume na mkataba.
3.      Kueleza sababu za kuwapa mashamba makubwa wawekezaji wa kigeni na kuwanyanyapaa wafugaji wa asili kinyume cha sheria.
4.      Kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji ambayo mara kadhaa imesababisha uvunjifu wa amani na umwagaji damu miongoni mwa wananchi.
5.      Kujenga viwanda vya kusindika nyama katika mikoa ya wafugaji ili kuongeza thamani ya bidhaa ya nyama na hivyo kukuza uchumi.
6.      Kuweka wazi kiasi cha fedha kinachopatika kama mrahaba kutokana na uvuvi katika bahari kuu, pamoja na fedha za leseni kwa meli zinazofanya uvuvi katika ukanda wa bahari kuu.

Bonyeza Read More Kuendelea

Serikali yaomba uraia wa nchi mbili kwenye Katiba

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeomba suala la uraia wa nchi mbili liwekwe kwenye Katiba mpya ili kuwawezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Hayo yalisemwa jana bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Benard Membe, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake.

Membe alisema Watanzania wanaoishi nchi za nje wanaathirika sana na suala la uraia wa nchini mbili kwa kuwa kutokuwa na uraia wa nchi mbili kunawafanya wakose ajira za kueleweka, huduma za afya, elimu na kushindwa kuchukua mikopo katika taasisi za fedha kama wenzao wa nchi mbalimbali.

Alisema Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni alikutana na Watanzania wanaoishi Ufaransa na Uholanzi na kuwahakikishia kuwa serikali yake inatambua na kuthamini michango yao hivyo kuwahimiza wakumbuke nyumbani.

Membe alisema katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwahamasisha Watanzania hao wawekeze kadri ya uwezo wao na wavutie washirika wao kuja kuwekeza hapa nchini.

Kuhusu changamoto kwenye balozi zake, Membe alisema ni za kiutawala na zingine ni za kibajeti kama ilivyoelezwa hivi karibuni katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),.

Alisema ubalozi wa Tanzania nchini Abu Dhabi na Muscat zilipata hati zenye shaka kufuatia matumizi mabaya ya fedha zilizotokana na makusanyo ya maduhuli.

Membe alisema kwa upande wa Abu Dhabi, hati hiyo yenye shaka ilisababishwa na Mhasisbu wa Ubalozi mdogo Dubai kupeleka kiwango pungufu benki kwa kiasi cha Dola za Marekani 20,000 ambazo ni sawa na Sh. milioni 33.

Kwa upande wa Muscat, Waziri Membe alisema maduhuli ya kiasi cha fedha za Oman 20,965 hazikupelekwa benki ndani ya wakati uliostahili kama kanuni za fedha zinavyoelekeza.

Alisema katika kukabiliana na changamoto hizo, hatua za kinidhamu zimechukuliwa kwa mujibu wa sheria za UAE  za kukata mshahara wa mhasibu huyo kila mwezi ili kulipa fedha zilizopotea.

CHADEMA yaahidi kujenga zahanati Tingeni

MRATIBU wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ametoa ahadi ya kujenga zahanati ya kata ya Tingeni katika jimbo la Muheza.
Bahweje alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Tingeni, Omary Kanyau, uliofanyika kijiji cha Ukoka.
Alisema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa huduma za afya kwani zilizopo ziko mbali na kwamba chama hicho kina mipango endelevu na wananchi hao.
Akizungamza kwa niaba ya wakazi wanaoishi katika kata hiyo, Shaban Salim, alisema kwa muda mrefu wanateseka bila kupata huduma za afya, hivyo kuwalazimu kwenda kutibiwa katika hospitali teule ilioko wilayani Muheza.
Salim alisema katika kata hiyo mbali na huduma za afya kuna tatizo la daraja ambapo likijaa maji huwezi kuvuka kwenda upande wa pili kitendo kinachopelekea watoto wanaosoma shule katika maeneo hayo kushidwa kuhudhuria masomo kutokana na daraja hilo kujaa maji.

Marekebisho ya hotuba ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje

Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha CUF....na kuishia na maneno…Israel Liberal ‘ sasa isomeke:
“Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International). Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal International Mwaka 1997.
Mwaka huo huo Liberal International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini Uingereza.
Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the rules of equality to sexual minorities and the recognition that homesexuality and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”. Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.
Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org)  kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja. Kupitia umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………”
Ezekiah Dibogo Wenje
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

30 Mei 2013

Thursday, May 30, 2013

CHADEMA kanda ya Kaskazini yagawa pikipiki za kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali  kufanya mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:
1.      Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha  ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2.      Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.
3.      Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.
4.      Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.
5.      Kujenga kitega uchumi katika kiwanja  cha Tanzania kilichopo Dubai na kukiendeleza kiwanja namba 19  tulichopewa bure na Serikali ya Uingereza kilichopo Uingereza (Central London) ambavyo vimekuwa maficho ya wezi kwa kutoendelezwa kwa muda mrefu na kusababisha Serikali za nchi hizo kutaka kutaifisha viwanja hivyo.
6.      Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za balozi zetu nchini China, na Uingereza kutoa hati za kusafiria kwa mataifa mengine hasa ya Afrika Magharibi ili kubaini ukweli na kuliondolea taifa aibu kutokana na tuhuma hizi.
7.      Kukarabati jengo la ubalozi wetu nchini China ambalo lilikuwa na nyufa na kuvuja nyakati za mvua, na kununua samani  na vifaa vya ofisi kama mashine za nukushi na za kurudufu ambazo zilikuwa hazipo,
8.      Kununua magari mapya ya ofisi ya ubalozi wetu nchini China kwa kuwa  magari matatu yaliyokuwepoyalikuwa yameshapitiliza muda wa miaka 10 ambao kwa mujibu wa sheria za China hayapaswi kutumika tena,
9.      Kupeleka mwambata wa kiuchumi (economic attaché)  nchini China ili kufuatilia fursa mbalimbali za kiuchumi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kutokana na mahusiano makubwa ya kibiashara  kati ya nchi yetu  na China
10.  Kuwawekea zuio wahusika wa kashfa ya rada kuwa viongozi wa shughuli za kiserekali ili walau kuonesha uwajibikaji wa kimaadili (moral accountability) baada ya kushindwa kuwawajibisha kisheria, ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kwamba dola imetekwa na mafisadi.
11.  Kuchunguza na kuwachukulia hatua watanzania (wafanyabiashara na wanasiasa) waliotorosha kiasi kikubwa cha fedha za nchi yetu (zaidi ya shilingi bilioni 315) na kuzificha katika mabenki ya uswisi
12.  Kutoa mchanganuo wa jinsi fedha za rushwa ya rada (chenji ya rada) zilivyotumika
13.  Kueleza bayana faida za kiuchumi tunazopata kama taifa kwa kushirikiana na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuthibitisha kwamba mashirikiano hayo hayatumiki kupora rasilimali za nchi yetu kwa hila ya “uwekezaji”
Mheshimiwa Spika, kabla sijajielekeza kwenye mambo mahsusi kwa kipindi hiki cha bajeti ya 2013/2014, napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kuitaka Serikali kutoa majibu mbele ya Bunge hili tukufu, kwamba imetekeleza kwa kiwango gani masuala yaliyoorodheshwa hapo juu, tuliyoitaka iyatekeleze (moja baada ya jingine) kwa mwaka wa fedha unaomalizika wa 2012/2013?

Bonyeza Read More Kuendelea

Upelelezi kesi ya Lema wakamilika

Upelelezi wa kesi ya kuchochea kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani katika Chuo cha Uhasibu Njiro  inayomkabili Mbunge  wa Arusha Mjini Godbless Lema umekamilika.Wakili wa Serikali, Eliainenyi Njiro, alieleza hayo jana wakati akiomba tarehe nyingine ya kusikilizwa shauri hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Devotha Msofe.
Aliomba kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Julai 2 kwa ajili ya kumsomea Lema maelezo ya awali.
Njiro alieleza kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Kwa upande wake, Hakimu, Msofe alikubaliana na upande wa Jamhuri pamoja na Wakili wa Lema ambaye ni  Humphrey Mtui kuwa kesi hiyo ipelekwe tena mahakamani hapo Julai 2 mwaka huu, kwa ajili ya mshtakiwa Lema kusomewa maelezo yake ya awali yanayomkabili katika kesi hiyo.

Slaa: Simchukii JK

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema hamchukii Rais Jakaya Kikwete kwa sababu ya dini yake bali kwa udhaifu wa serikali anayoiongoza.
Alisema udhaifu wa serikali anayoiongoza ndio umechangia maisha ya Watanzania yaendelee kuwa magumu licha ya Tanzania kubarikiwa rasilimali nyingi.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana Mbagala jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa hadhara wa kumnadi Cusbert Gwata, anayewania udiwani wa Kata ya Mianzini.
“Sina chuki na Rais Kikwete kama baadhi ya waeneza propaganda chafu wanavyofanya…watu wengine wanajaribu kupindisha kuwa namchukia kwa sababu ya dini yake, suala hapa si dini, suala ni kwamba yeye kama rais hana uwezo wa kuongoza.
“Anashindwa kusimamia na kutawala, kama mtu hana uwezo hakuna neno jingine wala mbadala wa kusema hayo…ni dhaifu tu,” alisema Dk. Slaa.
Alisema serikali ya CCM imekuwa ikijitahidi kutengeneza propaganda mbalimbali ikiwamo tofauti za kidini baina ya viongozi na makada wa upinzani dhidi ya watawala.
Alibainisha kuwa lengo la propaganda hizo ni kuficha udhaifu wao na kuwasahaulisha Watanzania wanaoteseka na mgawanyo wa rasilimali unaofanywa na serikali iliyopo madarakani.
Alisema hatamung’unya maneno wala kusita kuukosoa udhaifu wa serikali iliyopo madarakani kwakuwa akinyamaza ataifanya iendelee kuwatesa na kuwanyonya wananchi.
Alisema Watanzania wanapaswa kukumbuka mifano hai ya watu waliofanya kazi zao bila kuhusishwa na tofauti za dini walizonazo kuwa ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Dk. Slaa alisema kama angekuwa anawakosoa watu kwa sababu ya dini zao, basi asingemtaja Rais mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, katika orodha ya mafisadi.

Bonyeza Read More Kuendelea

Katibu CHADEMA adakwa kwa ugaidi

KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mtwara, Felician Melikisedeki, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa muda wa siku 10 bila kufikishwa mahakamani.
Melikisedeki inadaiwa anaandaliwa mashitaka ya kutaka kufanya ugaidi huku akizuiwa kuonana na watu walio karibu naye akiwemo mwanasheria wake.
Kada huyo amepokonywa simu yake ya kiganjani na polisi wanaodai imetumika kupiga picha nyumba ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na serikali waliojenga mkoani Mtwara.
Taarifa kutoka mkoani Mtwara zinaeleza kuwa Melikisedeki, alikamatwa Mei 17 mwaka huu, siku iliyodhaniwa ingesomwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Vyanzo vyetu ndani ya Jeshi la Polisi mkoani humo vimeiambia Tanzania Daima, kabla ya kukamatwa kwa Melikisedeki, lilikuwa likimfuatilia kwa hofu ya kuwashawishi wananchi mkoani humo kutenga muda wa kusikiliza bajeti ya wizara hiyo.
“Siku ile makachero wawili walikuwa wanamfuatilia na Melikisedeki akiwa katika moja ya grosari alipigiwa simu akasogea pembeni kwenda kusikiliza, kwa kuwa pale kulikuwa na kelele nyingi mmoja wa wale askari akamfuata lakini hakumuona,” kilisema chanzo chetu.

Bonyeza Read more Kuendelea

Asasi, Vyama na Makundi sasa ruksa kuunda Mabaraza ya Katiba

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa mwongozo unaoruhusu kuanza rasmi kwa uundwaji wa Mabaraza ya Katiba ya asasi, taasisi na makundi mbalimbali kwa lengo la kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya katiba inayotarajiwa kutolewa na Tume hiyo hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mwongozo ulitolewa na Tume hiyo leo (Jumatano, 29 Mei, 2013) na kusainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba, mwongozo utatumika kwa miezi mitatu kuanzia keshokutwa, Juni 1 hadi Agosti 31 mwaka huu.

“Mabaraza haya ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana yatajadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba,” amesema Jaji Warioba na kuongeza kuwa maoni hayo yanaweza kuwasilishwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa njia ya randama, barua, andiko, muhtasari wa makubaliano.

Mwongozo huo, ambao utachapishwa katika magazeti mbalimbali ya siku ya Alhamisi (Mei 30, 2013) na kurudiwa tena Jumatatu (Juni 3, 2013), pia unapatikana katika tovuti mbalimbali ikiwemo ya Tume hiyo (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume hiyo (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).

Kwa mujibu wa maelezo ya Jaji Warioba katika mwongozo huo, mabaraza hayo ya taasisi yanaundwa kwa mujibu wa kifungu cha 18 (6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kinachoitaka Tume kuruhusu Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wao kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwa Tume.

Katika mwongozo huo, Jaji Warioba ametaja taasisi zinazoweza kuunda Mabaraza hayo kuwa ni pamoja na Jumuiya ya Kidini, Chama cha Siasa, Asasi ya Kiraia, Taasisi ya Elimu ya Juu, Chama cha Wafanyakazi, Chama cha Wakulima, Chama cha Wafugaji, Chama cha Wanahabari na Baraza la Watoto.

Taasisi nyingine zinazoweza kuunda mabaraza hayo ni taasisi ya Wafanyabiashara, Mabaraza ya Wanawake, Taasisi ya Kitaaluma, Baraza la Vijana, Baraza la Wazee, Jumuiya ya Kijamii (CBO) na Chama cha Waajiri. Nyingine ni Chama cha Wanasheria, Umoja wa Watanzania waishio Nchi za Nje, Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, na Kundi au makundi ya watu wenye malengo yanayofanana au wale wenye mahitaji maalum katika jamii.

Kuhusu gharama za uendeshaji, mwongozo huo unaelekeza kuwa Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo Yanayofanana, yatagharimia taratibu zote za uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba hayo.

Kwa mujibu wa Jaji Warioba katika mwongozo huo, ili kuiwezesha kuratibu kwa ufanisi mchakato wa kukusanya maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, kila Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana yatakayounda Mabaraza ya Katiba itatoa taarifa ya maandishi ya kusudio la kuunda, kuendesha na kusimamia Mabaraza ya Katiba.

Taarifa hiyo itawasilishwa katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba moja kwa moja – Makao Makuu, Mtaa wa Ohio - Dar es salaam au Ofisi Ndogo Mtaa wa Kikwajuni Gofu Jengo la Mfuko wa Barabara Zanzibar. Taarifa pia inaweza kutolewa kwa Tume kupitia S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar.

Shehe apasua jipu la udini mkutano wa CHADEMA Uwanja wa Zakhem Mbagala

Aliwataka wananchi wa Kata ya Mianzini, Mbagala, Temeke Dar es Salaam kutofanya makosa kusikiliza propaganda za udini za CCM na kile chama kingine walichoungana nacho, Shehe Juma Mwipopo ametoa kauli nzito hapa akisema Serikali ya CCM ndiyo imeleta chokochoko zinazoendelea nchini.

Amesema kuwa siku zote viongozi wa CHADEMA wamesimamia na kuzungumzia maisha ya watu, si ukristo wala uislamu wao.

Amesema kule bungeni, Makamanda wa CHADEMA, chini ya uongozi wa Mwenyekiti na KUB Mbowe, akina Mnyika au Zitto hawazungumzii ukristo wala uislamu wao, bali maisha ya Watanzania, maisha ya binadamu, maendeleo ya watu.

Amesema kama ni udhalilishaji wa dini, na hasa viongozi wa kiislamu, CCM na serikali yake ndiyo wanaongoza

"Waislamu wenzangu ninyi ni mashahidi, alipokufa Michael Jackson, Rais Kikwete alimpigia simu Spika wa Bunge, Sitta asimamishe bunge ili kuomboleza, lakini bunge hilo hilo halikuomboleza kifo cha Naibu Mufti, Shehe Gorogosi...mnakumbuka namna ambavyo serikali hii ya CCM ilimzika Steven Kanumba, lakini hawakuweza hata kuhudhuria kwenye msiba wa Shehe Gorogosi ambaye alikuwa naibu mufti wetu...juzi juzi hapa mmeona msanii Lulu alituhumiwa kesi nzito ya mauaji, baadae kapata dhamana, lakini Shehe Ponda kanyimwa dhamana.

"Mnajua Watanzania wenzangu, Shehe Ponda alipokamatwa na kunyimwa dhama visivyo na serikali ya CCM watu wa kwanza kuzungumzia uminywaji huo wa haki walikuwa ni CHADEMA, wajumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando na Profesa Abdalla Safari, wakasema hiyo ni kinyume cha haki na sheria za nchi. Majuzi pia mmesikia Zitto kazungumza bungeni, akionesha namna ambavyo Waislamu wamenyanyaswa, ikiwemo tukio la Mwembechai, Zitto kazungumza Jumatano, Alhamis,onda kaachiwa mahakamani.

"Hivi ndivyo CHADEMA wanafanya kazi, chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wetu hapa, Dkt. slaa, wanazungumzia haki na ukweli kwenye maisha ya watu, maisha ya Watanzania. Wamepinga ufisadi. Mambo haya yote uamezungumziwa katika vitabu vyote vya dini, kupigania haki, kupigania ukweli, kupinga dhuluma, ufisadi na wizi. Hii ndiyo kazi ya CHADEMA chini ya viongozi wetu makini. Msikubali kudanganywa na CCM na serikali yake na CUF. " alisema Shehe Mwipopo ambaye ni Katibu wa CHADEMA, Wilaya ya Ukonga.
Zitto aomba msaada wa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema, amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron akimwomba kufuta sheria ya nchi yake inayowalinda watoroshaji wa fedha za umma wa nchi mbalimbali.
Zitto pia amemwomba Cameron kuzishawishi nchi nyingine tajiri kuwa na sheria za aina hiyo ili kudhibiti mafisadi wa nchi zinazoendelea.
Hatua hiyo ya Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema upande wa Tanzania Bara, ni mwendelezo wa juhudi zake za kupambana na mafisadi ndani ya Serikali wanaodaiwa kuweka katika benki za nje kiasi cha dola za Marekani milioni 196 (sawa na Sh323 bilioni).
Zitto amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia kuwa Waziri Mkuu Cameron atakuwa mwenyeji wa Kundi la Nchi Tajiri Duniani linalojulikana kama G-8 ambalo litakutana Lough Erne, Uingereza kuanzia Juni 17–18. Cameron ndiye atakuwa Mwenyekiti wa mkutano huo.
Novemba mwaka jana, Mbunge huyo alipeleka hoja binafsi bungeni akitaka iundwe timu maalumu kwa ajili ya kufuatilia kiasi cha Sh 323 bilioni ambazo zimethibitika kufichwa Uswisi.
Zitto aliikabidhi barua hiyo Jumatatu ya wiki hii kwa Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose, akimwomba aiwasilishe kwa Waziri Mkuu Cameron, kuelezea kilio cha Watanzania kuhusiana na fedha hizo.
Alisema sheria hiyo ina athari kubwa kwa maisha ya Watanzania wengi maskini na Afrika kwa ujumla, ambapo alisema anaamini sheria inayotaka uwazi itapitishwa kwenye mkutano wa mataifa manane tajiri yenye viwanda duniani, maarufu G-8, utakaofanyika mwezi ujao.
Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alisema kuwa ana taarifa kuhusu barua hiyo iliyoandikwa na Zitto kwenda kwa Cameron kuhusu shinikizo la Serikali kufanya mchakato wa kurudisha fedha zilizofichwa nje ya nchi.
“Tunafanya kazi na siyo kuzungumza ovyo kila mahali au kila hatua tuliyofikia, ila tunafanya kazi masaa yote, Watanzania wasubiri tu hatua tutakayofikia na tukiona tumejiridhisha tutawaambia nini kimefanyika,” aliongeza Werema.

Mheshimiwa Zitto Kabwe akikabidhi barua kwa Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Dianna Melrose inayokwenda kwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

Ndugulile CCM, Kama Mpinzani, akataa kutishiwa Nyau!

KAMA kuna Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayetakiwa kupokewa Kishujaa akirudi jimboni kwake toka bungeni kana kwamba ametoka vitani na ameshinda vita; basi ni Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile.
Sababu zinazomfanya Mbunge Ndugulile apokewe kishujaa na wananchi wake jimboni si ngeni bali ni ile aliyowahi kusema awali kwamba, Yuko tayari kufa kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa Jimbo lakela Kigamboni si wapiga kura tu.
Safari  hii Ndugulile, akiwa na sura inayompendeza kuwa Mpinzani alithubutu kukataa ambazo yeye aliziita Porojo za Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaujuka na Wizara yake akipinga wananchi wake wa Kigamboni kutofaidika na Mradi wa Makazi Mapya na kuingia mitini kwenye kikao.
Ikikumbukwa April 8, mwaka huu Dk. Ndugulile, aliapa kuwa yupo tayari kufa kwa ajili ya wananchi wa Kigamboni na haogopi vitisho vya baadhi ya wana CCM wanaohoji uhalali wa uanachama wake, kwa kile kilichoonekana na kuwatetea wananchi wake.
Alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika uwanja wa Swala, Kigamboni jijini Dar es salaam, Mbunge huyo alisema vitisho vya watu hao vinatokana na hatua yake ya kupinga dhuluma katika mradi wa mji mpya wa Kigamboni.
Dk. Ndugulile alisema kamwe hawezi kuzibwa mdomo kwa kuwatetea wananchi wake waliompigia kura na kumuamini na aliongeza kuwa ana uwezo wa kuwatetea na kuwaletea maendeleo ndani ya jimbo hilo, hata kama kuna watu wanasema, “Ukitaka Ubaya nchini Tanzania dai haki yako Uone!”.
siku hiyo ambayo alihutubia kwa staili ya kuwauliza maswali wananchi, Mbunge huyo alisema wananchi wa Kigamboni bado hawajaelewa mambo muhimu katika mradi huo na ndiyo maana kila anapowauliza kama wanafahamu mradi huo lini utaanza, sehemu utakapoanzia na kiasi cha fidia, hawakuwa na majibu.

alisema "Angalieni wenyewe, nimewauliza maswali lakini hakuna jibu, hata mimi pia sijui kwa sababu sina nyaraka zozote zinazoonyesha vitu hivyo,"
Aliongeza kusema maswali kama hayo amewauliza viongozi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi akiwamo Waziri Profesa Anna Tibaijuka, lakini cha kusikitisha wote hawakufahamu.
"Sipo hapa kupinga mradi wa mji mpya, ninayosema ndiyo maneno yenu ninyi wana-Kigamboni, sasa asiwepo mtu akaanza kupotosha na kuniona mimi napinga Ilani ya Chama changu," alisema.
Hata hivyo, alisema tayari suala lote la mji mpya wa Kigamboni alilipeleka katika vikao vya Chama ili kujadiliwa kwa umakini, ambapo aliwataka wananchi wake kusubiri uamuzi wa vikao hivyo
hata hiyo alizungumzia fidia ya Sh. milioni 145 kwa ekari iliyotangazwa na Waziri Prof. Tibaijuka, ambayo Dk. Ndugulile alisema fidia hiyo ni kiini macho kwa sababu wakazi wengi wa Kigamboni hawana maeneo yenye ukubwa kama huo
Nanukuu "Sisi wakazi wa Kigamboni tunaishi watu ishirini ndani ya ekari moja, sasa ukigawanya kiasi hicho kwa idadi hiyo, ni wazi mwananchi wa kawaida hatapata fidia inayolingana na thamani ya eneo lake. Hii ni kutudanganya tu," aliongeza
Siku hiyo hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema, bila kumung’unya maneno aliwaambia wanachama wa CCM kuwa Mbunge huyo kijana, ni mwanachama mtiifu wa CCM na hawezi kuondoka kwenye chama hicho hata kama kuna watu wenye nia mbaya wanataka afanye hivyo.
Sikunjema alidai kama mivutano ilitokana na uwepo wa mradi wa mji mpya wa Kigamboni, hivyo chama hicho kiliamua kuingilia kati kujadili changamoto mbalimbali zilizoukabili mradi huo
Katika kujadili makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi iliyowasilishwa na Prof. Tibaijuka, Ndugulile alimshambulia waziri akisema anatoa porojo kwamba yeye (Ndugulile) aliingia mitini katika kikao cha madiwani ambapo ukweli halisi alikuwa safari ya kikazi.

Aidha Pamoja na Spika Anne Makinda kujaribu kumtisha Ndugulile ili alainike au kuogopa asiendelee kuwatetea wananchi wa Kigamboni, Mbungu huyo Kijana alikataa kutishiwa Nyau na kuendeleza mapambano hadi Spika akalazimika kuitaka Serikali ikake na wananchi wa Kigamboni iridhiane nao.

Bryceson Mathias

Waziri Kabaka; Wawekezaji wanajifanya wako juu ya Watanzania.

INGAWA Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka (MB) kasema mifuko ya hifadhi iko kwenye hali nzuri na ni endelevu, Ingawa kuikweliiko kwenye hali mbaya, mfuko wa Pensheni ya wafanyakazi (PPF) ni Janga kwa wastafu na wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo.
Siafikiani na Waziri Kabaka kwamba Migogoro sehemu za kazi imepungua kwa kutumia maridhiano ya chombo cha kutatua Migogoro(CMA), bali ndiyo kwanza imeongeza na tena ni mibaya kuliko ile ya awali kwa sababu Wawekezaji wanajifanya wako juu ya watanzania.
Katika michango ya Wabunge kwenye Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Kazi na Ajira, waliitaka Serikali na Wizara Ichukue hatua Kali dhidi ya Mifuko inayochelewesha Michango ya Wafanyakazi, Jambo ambalo Waziri Kabaka alikiri kuwapo kwa tatizo hilo.
Nimsadie Waziri Kabaka, Waajiri na hasa Wawekezaji ambao hivi sasa wanajifanya kuwa wako Juu ya Wafanyakazi na Watanzania, wamekuwa na nguvu ya kuwadhulumu na kukaa na Michango ya Wafanyakazi au Mafao ya Wastaafu, kwa sababu ya Kiburi ya Fedha.
Kiburi ya Fedha, imesababisha baadhi ya Watoa maamuzi tangu Ngazi za Wizara ya Kazi kuwa kama Vipofu wasioona udhalimu na Viziwi wasiosikia, Malalamiko ya aina yoyote inayotolewa na wafanyakazi na Wastaafu, jambo lililopiga hodi hadi Serikali Kuu.
Mfano; Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kupitia Mfuko wa PPF, kwa miaka kadhaa amekuwa hapeleki michango ya wafanyakazi wake tangu alipobinafshiwa Kiwanda, asilimia 5% waliyokatwa wafanyakazi kwenye mishahara, na 15% anayotakiwa atoe mwajiri.
Kimsingi wafanyakazi zaidi ya 100 wa mtibwa, wameshafariki bila kupata mafao yao, ambapo hata wajane au wagane waliobakia, wameendelea kunyanyasika wasiyapate mafao hayo hadi leo, na waliopata kiasi, wamepewa kwa mafungu kama Nyanya za sokoni, fedha zikitumika.
Inatafsirika kuwa, baadhi ya vigogo na wastaafu serikalini wenye sauti na hisa ya uwekezaji huo, cha kusikitisha wamehusishwa katika dhuluma na manyanyaso ya haki za wafanyakazi na wastaafu hao, ambapo kwa dhuluma hizo huko mbinguni tutakuwa Kuni.
Kama kuna mfuko ambao siupendi moyoni mwangu na hata kuuona, basi ni PPF. PPF wameshiriki kudhulumu haki za wafanyakazi wa mtibwa. Kwa muda mrefu nadhani ni kuwaheshimu baadhi ya vigogo wastaafu, kiasi wamepora michango ya wafanyakazi na wastaafu.
Wengi wao wamekufa kwa kihoro na mwingine aliyekuwa alipwe Mil. 13/- kufanya kazi miaka 14; alipwe Mil. 2.5/-, jambo lililowafanya vijana wengi wenye nguvu kuacha kazi na kufanya kazi za kujiajiri au kwenda kwingineko; mmoja wao  ni Mkurugenzi wa kufuatilia Mwenendo wa Bunge Marcossy Mgweno.
Sisemi kama wanavyoambiwa viongozi na wananchi nchini wasioijua mtibwa ilivyo. Ninao ushahidi na ninaweza kuutetea. Utetezi wa awali Mtibwa 2005 ilihukumiwa na Mahakama ya kazi kumlipa kila mfanyakazi aliyedai Sh. 500,000/- kwa kuchewesha Michango.
Ieleweke, Mgeni aliyelala Kiangazi nyumba inayovuja, hawezi kujua kuvujiwa na adha ya Mvua katika nyumba hiyo; Akiamka kuendelea na safari, ataishia kuisifu kwa kumtunza usiku ule, lakini ingekuwa wakati wa Mvua angeilaani.
Aidha Waziri Kabaka Mwenyewe, akiwa Naibu Waziri, alishindwa kutatua migogoro na maatatizo ya wafanyakazi na wastaafu wa Mtibwa mara mbili, ambapo alijua dhuluma na unyanyasaji unaoendelea kufanyika, huku viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakila asali.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA KWA MWAKA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa spika, mwaka jana nilianza hotuba yangu kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki  wa wale wote waliofariki dunia kwa ajali ya mv skagit, mwaka huu naomba nianze hotuba yangu kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa wale waliofariki kwa ajali nyingine ya kizembe ya kuanguka kwa ghorofa la Dar Es Salaam. Aidha, mwaka jana nilianza kwa kutoa pole kwa Mh. Joseph selasini kwa kufiwa na baba yake na mwaka huu nianze pia kwa kutoa pole kwa Mh. mchungaji Israel Natse kwa kufiwa na baba yake mzee Yohana Natse. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake , mahali pema peponi.

Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi wala ushindani kuwa Serikali yoyote makini duniani huweka sera na mifumo thabiti ya kuhakikisha kuwa ajira za kutosha zinatengenezwa, mazingira ya kazi yanaboreshwa na wafanyakazi wanalipwa ujira na mishahara yenye staha, si tu kwaajili ya kuwawezesha kumudu gharama za maisha, bali pia kuwapa morali wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya taifa.
Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza kuwa  Taifa lolote duniani ambalo haliwezi kutengeneza ajira na hivyo kuwafanya vijana wake wengi wenye uwezo wa kuajiriwa kuzurura mitaani, na wale walio vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu ya Serikali kushindwa au kupuuza kugharamia masomo yao; sote tunatambua kuwa Taifa hili  limejaliwa rasilimali nyingi za utalii na madini ya thamani, lenye vyanzo vingi vya kodi na mapato, lakini limegubikwa na migogoro mingi, ya mara kwa mara na isiyokwisha, ya wafanyakazi wanaodai haki na mafao yao halali, huku wakiishia kunyamazishwa kwa kauli laini zenye matumaini hewa; Kwa namna yoyote ile taifa hilo, ni kielelezo cha nchi inayoongozwa na Serikali isiyo na vipaumbele, yenye viongozi wasiojali na wanaotekeleza sera wasizozijua au zilizoshindwa.

Bonyeza Read More Kuendelea

Wednesday, May 29, 2013

MAONI NA MAPENDEKEZO YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) JUU YA RASIMU MUONGOZO ULIOTOLEWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KUHUSU MABARAZA YA KATIBA YA ASASI, TAASISI NA MAKUNDI YENYE MALENGO YANAYOFANANA.

1.0. UTANGULIZI

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83 (kifungu cha 18 (3)) imetoa wajibu kwa tume wa kuunda Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume.

Kifungu cha 17 (8) kinaeleza kuwa, isipokuwa kama mazingira yatahitaji vinginevyo, Tume itabuni utaratibu unaofanana ambao utatumika kila upande wa Muungano.

Kifungu cha 18 (6) kinaeleza aina nyingine ya Mabaraza ya Katiba kwa kueleza kuwa Tume inaweza kuruhusu Asasi, Taasisi au Makundi ya Watu kuwasilisha maoni yao kuhusu Rasimu ya Katiba.

Ikumbukwe kwamba Kamati Maalum ya CHADEMA  ilikutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 7 Januari 2013 kuwasilisha maoni ya CHADEMA kuhusu katiba mpya kama ilivyoalikwa lakini pia kutumia fursa hiyo kuwasilisha mapendekezo ya CHADEMA kuhusu marekebisho na maboresho yanayohitajika kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba ili kupata katiba bora.
Tarehe 31 Januari 2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa taarifa kwamba imeamua kuwa Mabaraza ya Katiba yatakuwa katika makundi mawili yafuatayo: Mabaraza ambayo Tume itayasimamia na kukusanya Maoni (Mabaraza ya Katiba ya Wilaya – Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa) na Mabaraza ambayo Tume haitayasimamia. Mabaraza hayo yatajisimamia yenyewe na kukusanya maoni yatakayowasilishwa kwenye Tume kwa mujibu wa maelekezo. (Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu).

CHADEMA baada ya kupitia muongozo huo na kwa kuzingatia kuwa tayari tume ilishafanya uamuzi kuwa mabaraza ya katiba yatakuwa ya wilaya, tarehe 14 Februari 2013 kiliwasilisha maoni na mapendekezo yake kuhusu uteuzi wa wajumbe  ambayo kwa sehemu kubwa hayakuzingatiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na hivyo kusababisha matatizo makubwa katika mchakato mzima wa uteuzi wa mabaraza ya katiba ya wilaya.
Kufuatia hali hiyo katika Maoni ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tulitangaza kwamba CHADEMA itajitoa ushiriki wake katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo yafuatayo hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2013:
“Mosi; Kufutwa kwa uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata, na badala yake wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC;

Pili: Serikali ilete mbele ya Bunge hili tukufu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatayofanyia maeneo yafuatayo marekebisho.”

Bonyeza Read More Kuendelea

Spika Makinda azima hoja ya Mdee kuhusu umiliki wa mashamba makubwa

Spika wa Bunge, Anne Makinda jana aliizima hoja ya Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhusu umiliki wa mashamba makubwa yasiyoendelezwa wakati wa kujadili hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo ilihitimishwa bungeni jana.
Mdee alivutana na Spika Makinda wakati wa kujadili bajeti hiyo kifungu kwa kifungu, Mdee alipotaka kufahamu kauli ya Serikali kuhusu kampuni zinazomiliki ardhi bila kuziendeleza na hatua zinazochukua kuhakikisha zinarudishwa kwa wananchi.
Baada ya kuuliza swali hilo huku akisisitiza kutoa shilingi, Spika Makinda alimtaka kukaa chini kwa kuwa hoja yake haina mashiko ya kufanya hivyo na kwamba kama anataka aiwasilishe kama hoja binafsi.
“Kaa chini, nakwambia kaa chini,” alisema Makinda huku Mdee akionekana kuendelea kuzungumza... “Nasema kaa chini,” alirudia na Mdee kukaa huku akikipeperusha karatasi hewani kuonyesha kutokubaliana naye.
Awali, Mdee alisema shamba la Simanjiro ambalo Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza mwekezaji kupewa ekari 500 lakini Wizara ya Ardhi iliidhinisha ekari 25,000 ambazo mwekezaji hajaziendeleza zote wakati mashamba ya Kisarawe na mashamba ya mkonge Tanga ambayo wawekezaji wameyakopea fedha nayo hadi sasa hayajaendelezwa.
Alitaka kauli ya Serikali kuhusiana na hali hiyo na jinsi ya kurudisha mashamba hayo katika miliki ya umma. Mbunge mwingine aliyetishia kutoa shilingi ni Dk Faustine Ndungulile wa Kigamboni (CCM), akijikita katika suala la ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni akisema wananchi wake hawakushirikishwa katika mipango ya ujenzi huo.
Akijibu hoja hizo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema wananchi wameshirikishwa kikamilifu katika mchakato mzima na kuahidi kukaa na mbunge huyo pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kuzungumzia suala la Kigamboni.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye alisema kila mkazi atalipwa Sh35,000 kwa kila mita moja ya mraba na mwenye ekari moja atapata Sh141 milioni na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa mradi huo utakuwa wa maendeleo kwa kila mmoja.
Baada ya majibu hayo, Dk Ndungulile alisimama na kusema kuwa anakubali kurejesha shilingi hasa baada ya Waziri Tibaijuka kutamka kuwa wananchi wameshirikishwa na watashirikishwa katika kutatua mgogoro wa Kigamboni.
Spika Makinda aliwataka kushirikiana kutatua mgogoro wa Kigamboni ili mradi uanze. 

Sekondari ya Mpwayungu yafungwa kwa ukosefu wa Maji.

Walimu na Wanafunzi wa Sekondari ya Mpyayungu Kata hiyo Manispaa ya Dodoma, wanajiandaa kurudi makwao baada kulazimishwa kuwahi kufunga kutokana na ukosefu wa maji.
Malalamiko hayo yametolewa jana 28.5.13 na Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo, kutokana na baadhi yao kuanza kuumwa matumbo na kuhara kutokana na kutumia maji machafu wanayochota visimani.
Wakizungumza kwa masikitiko ya kuwahi kufunga wakati bado wana wana majaribio ya mitihani Wanafunzi na Walimu hao walimlaumu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Gabriel Hoya, kwa kushindwa kutengeneza Mashine ya kusukuma maji kwa sababu zisizoeleweka.
“Hii ni mara ya nne sasa walimu na wanafunzi wanapata adha za namna hii, ambapo hata viongozi wa Kata wanaonekana kutotilia maanani usumbufu unaowakabili walimu na wanafunzi katika masomo”. Alisema mmoja wa walimu aliyeomba asitajwe.
Mwandishi alimtafuta mwalimu mkuu wa Sekondari, Andew Honya, aliyekiri kuwepo kwa tatizo na kusema wanalazimika kufunga shule mapema kutokana na ukweli huo ambapo alisema wanaogopa magonjwa ya kuambukiza yasitokee shuleni hapo
Hata afisa elimu wa Shule za Sekondari wilaya ya Chamwino. Valentine Christopher, nimemuarifu na ameruhusu hatua hiyo na kuridhia ifanyike ili kuweka Kinga badala ya kukaribisha madhara.
Afisa Elimu Sekondari Christopher, alipotafutwa ajibu mkasa huo simu yake ilikuwa haipatikani, na  msaidizi wake, Hamisi Mapoto, pia hakupatikana, ambapo Afisa Elimu Msingi,  Scolar Kapinga, simu yake iliita lakini hatukuweza kusilizana kutokana na mwandishi kuwa juu ya mti ili apate mawasiliano.

BRYCESON NYEREGETE

PolisiCCM kwenye mkakati mzito wa kubambika kesi nyingine ya ugaidi Mtwara, gazeti la kesho kutumika

Wadau nyeti mbili usiku wa leo ambazo pro CHADEMA mnapaswa kujiandaa kuzikabili kama CCM wataendelea na mpango wao kama ulivyopangwa ufanyike kuanzia kesho.

Kwanza kesho Team Lowassa, CCM na polisi kupitia gazeti moja ambalo mmoja wa wahariri wake ni mtu unethical kupindukia na karibuni ameweka rekodi ya kujitenga na wenzake, wamepanga kutunga na kupika stori ikiwa ni mwendelezo wa kukipaka matope CHADEMA na issues za ugaidi.

Watamtumia mwana CCM mmoja kutoka Mbeya ambaye aliwahi kuwa CHADEMA kabla hajahama miaka takriban miwili iliyopita, baada ya kuuza 'ubunge' mara mbili, mara ya kwanza kwa kujifanya amekosea namna ya kutekeleza masharti ya kisheria.

Atanukuliwa na gazeti hilo akijitambulisha kuwa eti aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya CHADEMA, na katika kikao kimoja chini ya uenyekiti wa Kamanda Mbowe, walipanga mipango ya ugaidi.

Gazeti hilo litalotumika ni moja ya magazeti ambayo CCM, wakiwemo Team Lowassa na polisi wameamua kulitumia kusukuma agenda ya kukipaka matope CHADEMA na viongozi wake wakuu kwa kashfa za kupika, lengo ikiwa ni kuwahusisha viongozi wakuu wa chama hicho na hatimaye CCM watekeleze wanachokitaka.

PILI

Kwa takriban zaidi ya siku 10 sasa, polisi mkoani Mtwara wamekuwa wakimshikilia Kaimu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mtwara, anayeitwa Melikizedeki, nimefanikiwa kupata jina moja kwa hataka niliyokuwa nayo kuleta hii habari hapa jamvini.

PolisiCCM wa Mtwara walimkamata tangu Ijumaa ya Mei 17. Tangu wakati huo amenyimwa haki zake za msingi, ikiwemo kuonana na mwanasheria wake, hata wakati wa kuandikishwa maelezo yake! Hajaruhusiwa kabisa kukutana na ndugu zake. Mwanzoni hata chakula hakuwa akipewa. Hadi sasa kwa siku zote hizo, amenyimwa kabisa dhamana.

Hiyo tisa, kumi ni kwamba polisi walipomkamata walimyang'anya simu yake. Sasa baada ya kukaa nayo muda wote huo, wameikagua bila kuwepo mtu yeyote mwingine kama shahidi, wameshinikizwa wamfungulie kesi ya ugaidi na uchochezi, kisa eti kwenye simu yake wamekuta picha za nyumba ya Hawa Ghasia na George Mkuchika na meseji zingine.

Polisi wanatumika vibaya sasa, kuliko hata ile mipira...hivi kweli mtu unawezaje kuchukua simu ya mtu, umekaa nayo huko, hakuna anayejua umeifanya nini, umeingiza vitu gani, kisha huo ndiyo uwe ushahidi mahakamani? 

Habari zinasema kuwa hata ndani ya jeshi la polisi huko Mtwara wanabishana sana kupeleka hiyo kesi mahakamani. Wengine wachache waliobakiwa na akili za kupembua chenga, mchele na pumba, wanaopenda kutumikia jeshi hilo kwa weledi na taaluma na maadili, wanaona hicho kitu hakikubaliki. Walio mafisadi, polisiCCM wanasukuma kesi ifikishws mahakamani ikibidi hata kesho.

Ni mtu mgeni huko Mtwara, yaani si mzaliwa wa huko. Amekwenda kikazi. Asilia, kwao ni Kagera. Anaelezwa kuwa mtu mwenye msimamo kwa sababu anajua vitu. Lakini kinachoonekana ni kwamba baadhi ya viongozi wa CHADEMA wasiokuwa waaminifu huko Mtwara hasa ngazi ya wilaya wamemsaliti mwenzao. Kwanza walichelewa sana kutoa taarifa makao makuu ili hatua za haraka zichukuliwe.

Pili, baadhi yao wamekuwa hawatoi ushirikiano wa dhati kumsaidia Melikizedeki ambaye anatajwa kuwa mfanyakazi wa moja ya NGO inayoshughulikia watoto yatima. Viongozi hao hivi karibuni, wakati wa sakata la gesi lilipoibuka mara ya kwanza kabisa, walirubuniwa na watu wa usalama wa taifa wilayani na DC, wakaletwa Dar es Salaam kuonana na Waziri Mkuu, bila hata kukitaarifu chama chao na kushirikisha uongozi. 

Bwana Melikizedeki kwa kutambua msimamo wa chama hicho katika masuala yanayoweza kuonekana kuwa ni kuwasaliti Watanzania ambao kimekuwa kikiwatetea, akapinga hiyo move ya hao wenzake, kwenye vikao na hata hadharani katika mahojiano na redio. Wakamchukia.

Taarifa zinasema Makao Makuu wamechukua hatua ya kutuma wanasheria haraka kwenda Mtwara.

Ni hayo kwa leo, wakati kesho tukisubiri Gazeti la kuendelea kutumika na kuzidi kujitangaza kuwa ni 'adui wa umma' kwa kupika na kutengeneza stori.

CHADEMA walalamikia rafu Makuyuni

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, amelionya Jeshi la Polisi wilayani Monduli kutoendelea kutumika kukihujumu chama hicho katika uchaguzi wa udiwani Kata ya Makuyuni kama linavyofanya sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Golugwa alisema Jeshi la Polisi Monduli sasa linatumika kukamata vijana wote wanaodhaniwa wanakiunga mkono chama hicho kwa shinikizo la wanasiasa wakongwe nchini.
“Kuna vijana wamekamatwa Makuyuni tangu tulipozindua kampeni za uchaguzi za chama chetu baada ya kuonekana wakipeperusha bendera za chama… tuna ushahidi kuwa ni maagizo kutoka kwa mmoja wa vigogo wa CCM Monduli,’’ alisema Golugwa.
Aliliomba Jeshi la Polisi kutojitumbukiza katika kampeni chafu, kwani CHADEMA ina uwezo wa kujilinda na kupambana na hali zote.
Alifafanua kuwa wao kama chama tayari wanaanza kujipanga kupitia vijana wa chama hicho mkoani ‘Red Brigade’ kwa ajili ya kwenda kuwalinda viongozi Monduli na kupambana na wote watakaojaribu kuharibu kampeni za chama hicho.
Baada ya mkutano huo, katibu huyo aligawa pikipiki saba zenye nembo ya chama hicho kwa wilaya za Monduli na Arusha Mjini kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za chama.
Naye mgombea udiwani wa Makuyuni, Japhet Sironga, alisema baada ya kuonekana anaungwa mkono na wananchi sasa kumeanza kampeni chafu za ukabila Monduli na yeye japo ni Mmasai wa asili akibatizwa kabila ambalo si lake.
“Hali ya Monduli inabadilika kila kukicha sasa wananchi wanatishwa na kampeni za ukabila zinaendeshwa na kuhatarisha umoja wa wakazi wa Makuyuni, kuna watu wametishwa wasipotoa kura kwa CCM watalaaniwa,” alisema Sironga.

Tuesday, May 28, 2013

Mdee awavaa wenye mashamba makubwa

Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeorodhesha mashamba 36 yenye ukubwa wa maelfu ya hekta za ardhi ambayo wananchi waliporwa kimabavu na Serikali kwa kutofuata sheria na kisha kupewa wawekezaji. 

“Naamini taarifa hii itapelekea Bunge lako tukufu, kutoa au kufanya maamuzi yenye busara kwa manufaa ya taifa na wananchi wake,” alisema Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Halima Mdee, alipokuwa akisoma hotuba ya kambi hiyo kuhusu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2013/14. 

Pia Mdee alisema kuna mashamba sita ambayo taarifa za wawekezaji haziko wazi ama hazieleweki. 

Alitaja mashamba hayo kuwa ni Chawangwa ambalo lina  hekta 200 za ardhi ya Kijiji (1), lipo Kisarawe. Lilikuwa ni kwa ajili ya kilimo cha Jatropha lakini  halijaendelezwa, Euro Mine Export  Ltd ambayo shamba lake lipo Mikese mkoani Morogoro kwa ajili ya kilimo cha Jatropha.  

Mashamba mengine ni yaliyopewa ni kampuni ya Oxman Tanzania Ltd lililopewa Rufiji kwa ajili ya Kilimo cha Mpunga na lile lililopewa Kampuni ya Rubana ambalo lipo Mwanza kwa ajili ya kilimo cha Jatropha ambalo hata hivyo  halijulikani kwa maafisa kilimo wa  ardhi wa Wilaya. 

Makampuni mengine yaliyopewa mashamba na kushindwa kuendeleza ni Kampuni ya Synergy Tanzania Ltd iliyopewa shamba la hekta 20,000 huko Rufiji kwa ajili ya kilimo cha Mpunga, Tanzania Biodiesel Plant ambalo lina hekta 16,000 za shamba, ambalo lipo Bagamoyo. 
 
VIGOGO WA CCM
Mdee alisema Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, Brown Oleseya, ambaye amemilikishwa kiujanja ujanja hekta za kijiji 3425. 

Alisema licha ya kujipatia kiwanja hicho kiujanja ujanja, Oleseya amewafungia wananchi njia zote za chemchem za maji ya malisho ya mifugo. 

Alisema Agosti 31 mwaka 2009, Oleseya kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu walibadilisha matumizi ya shamba kutoka kilimo na ufugaji kuwa hifadhi ya kitalii. 
Alisema nyaraka zote anazozitumia kama ushahidi mwenyekiti huo, hazina uhalali wowote kisheria.

Mdee alihoji iwapo serikali kueleza kama iko tayari kuvunja majumba makubwa ya wenye fedha waliouziwa maeneo ya wazi kinyume na utaratibu nma kupewa hati na maofisa wasiowaamifu. 

“Serikali inatoa tamko gani juu ya kiwanja namba 856 cha Msasani Beach ambalo kwa mujibu wa ramani ya upimaji iliuosajiliwa namba 29331 ilikuwa ni kwa matumizi ya wazi?,”alihoji.
 
Alisema hali hiyo ilifanya njia ya mkondo wa maji kuelekea baharini imezibwa na mvua ikinyesha maeneo ya Warioba yanajaa maji.